Pata taarifa kuu
INTER MILAN-ITALIA

Inter Milan yamfuta kazi kocha wake mkuu, Frank de Boer

Klabu ya Inter Milan ya Italia, imetangaza kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo, Muholanzi, Frank de Boer, baada ya siku 85 tu toka alipokabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi hicho. 

Aliyekuwa kocha wa Inter Milan ambaye sasa amefukuzwa, Frank de Boer.
Aliyekuwa kocha wa Inter Milan ambaye sasa amefukuzwa, Frank de Boer. Reuters / Alessandro Garofalo Livepic
Matangazo ya kibiashara

Inter Milan kwa sasa iko kwenye nafasi ya 12 kwenye orodha ya jedwali ya timu zinazoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama Seria A, ambapo kipigo cha bao 1- 0 kutoka kwa klabu ya Sampdoria siku ya Jumapili, kilikuwa ni kipigo cha nne mfululizo katika mechi tano za ligi.

Beki huyu wa zamani wa kati wa timu ya taifa ya Uholanzi na aliyekuwa kocha wa Ajax, alikuwa akihusishwa sana kwenda kufundisha soka nchini Uingereza, ambapo alihusishwa na vilabu vya Everton na Southampton.

Inter MIlan inatarajiwa kucheza na klabu ya Southampton kwenye mchezo wa kombe la Europa League siku ya Alhamisi.

Klabu hiyo sasa imemtangaza kocha wa timu ya vijana, Stefano Vecchi kuiongoza kwa muda timu hiyo hadi pale atakapopatikana kocha mpya.

Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, kocha de Boer ameandika kuwa "kufanyia kazi program ya timu hii inahitaji muda" ambapo pia akawashukuru mashabiki wa Inter kwa kumuunga mkono.

Kabla ya kujiunga na Inter Milan, De Boer aliiongoza klabu ya Ajax kutwaa taji la ligi kuu ya nchi hiyo mara nne mfululizo lakini alipoteza nafasi hiyo msimu uliopita kwa mahasimu wao klabu ya PSV Eindhoven.

Alisaini mkataba wa miaka mitatu na Inter Milan mwezi August mwaka huu akiziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyewahi kuwa kocha wa Manchester City, Roberto Mancin.

Katika kipindi cha miaka 6 Inter Milan imeshashinda mataji matatu ya ligi ya Seria A, Coppa Italia na Klabu bingwa Ulaya chini ya kocha Jose Mourinho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.