Pata taarifa kuu
CCL-CL-CAF

Kitimtim mechi za kuamua nani kucheza fainali ya kombe la klabu bingwa na shirikisho Afrika

Mechi za hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la klabu bingwa barani Afrika na ile ya kombe la Shirikisho, zinatarajiwa kupigwa mwishoni mwa juma hili, ambapo timu zitakazofuzu hatua ya fainali zitajulikana.

Kocha wa timu ya ZESCO akisalimuana na mlinda mlango wa Sundwons, Denis Onyango, wakatik timu zao zilipokutana hivi karibuni.
Kocha wa timu ya ZESCO akisalimuana na mlinda mlango wa Sundwons, Denis Onyango, wakatik timu zao zilipokutana hivi karibuni. goal.com
Matangazo ya kibiashara

Katika mechi za kombe la klabu bingwa, klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, itakuwa nyumbani kuwakaribisha majirani zao klabuj ya ZESCO United, katika mchezo wa kufa na kupona kwa timu zote mbili.

Kwenye mchezo huu utakaopigwa Jumamosi ya September 24, kila timu itahitaji ushindi ili kusonga mbele, huku ZESCO wao wakihitaji angalau kupata goli moja tu kuongeza mlima kwa Sundwons ambayo nayo inahitaji ushindi wa bao moja kwa bila au zaidi ili kutinga hatua ya fainali.

Kwenye mchezo wa awali uliopigwa mjini Ndola, Zambia, timu ya ZESCO ilifanikiwa kupata ushindi wa nyumbani wa mabao 2-1.

mechi nyingine kwenye michuano hii, ni ile itakayozikutanisha timu ya Wydad Casablanca ambayo yenyewe itakuwa nyumbani kuwakaribisha waliowahi kuwa mabingwa wa taji hilo klabu ya Zamalek ya Misri, kwenye mchezo ambao Zamalek wanaingia uwanjani wakiwa na faida ya mabao 4-0.

Kwenye mchezo wa awali uliopigwa jijini Cairo, Zamalek walichomoza na ushindi mkubwa wakiwa nyumbani wa mabao 4-0, ushindi ambao unaipa wakati mgumu sana klabu ya Wydad Casablanca kurejesha mabao yote na pengine kuongeza ikiwa inataka kufuzu.

Baada ya mechi hizi za marejeano timu zitakazofuzu fainali ya michuano hii mikubwa kabisa baranik Afrika kwa ngazi ya vilabu, zitajulikana, maswali yanabaki je, ni Zamalek dhidi ya ZESCO? Au Wydad dhidi ya Sundowns? Wataalamu wa soka wanasema yote haya ytanawezekana baada ya dakika 90 kukamilika.

Baadhi ya wachezaji wa TP Mazembe ya DRC wakishangilia moja ya magoli ambayo timu yao ilifunga.
Baadhi ya wachezaji wa TP Mazembe ya DRC wakishangilia moja ya magoli ambayo timu yao ilifunga. goal.com

Kwenye kombe la shirikisho pia kutakuwa na mechi ambazo zitapigwa Jumapili ya September 25, ambapo klabu ya TP Mazembe ya DRC, itakuwa nyumbani kuwakaribisha Etoile du Sahel ya Tunisia kwenye mchezo mwingine ambao ni muhimu kwa timu zote mbili kwakuwa zinahitaji ushindi.

Katika mchezo wa awali mjini Tunis, Tunisia, timu hizi zilitoshana nguvu ya kufungana bao 1-1, matokeo ambayo yanaipa Mazembe nafasi ikiwa itapata angalau bao moja na zaidi huku pia Etoile nayo ikihitaji walau bao moja ama sare ya bao 1-1 ili kufuzu kucheza hatua ya fainali.

Mechi nyingine kuwania taji hili itazikutanisha timu ya FUS Rabat ya Morocco ambayo itakuwa nyumbani kuwakaribisha MO Bejaia ya Algeria, kwenye mchezo mwingine unaosubiriwa kwa hamu, kwakuwa kila timu inayo nafasi ya kufuzu.

Kwenye mchezo wa awali, timu hizi hazikufungana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.