Pata taarifa kuu
SOKA WANAWAKE

Jukwaa liko tayari kwa michuano ya AFCON wanawake nchini Cameroon

Bingwa mtetezi wa kombe la mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake, timu ya taifa ya Nigeria, itaanza kutetea ubingwa wake kwa kucheza na timu ya taifa ya Ghana, Mali na Kenya kwenye kundi B.

Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria ambao ndio mabingwa watetezi
Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria ambao ndio mabingwa watetezi cafonline.net
Matangazo ya kibiashara

Wenyeji Cameroon wamo kwenye kundi A na watakabiliana na Misri kwenye mchezo wa ufunguzi, tarehe 19 ya mwezik November mwaka huu mjini Yaounde, Cameroon.

Afrika Kusini na Zimbabwe, ambao wote walishiriki kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, nchini Brazil, wanafunga dimba ya orodha za timu kwenye kundi lao.

Fainali za michezo ya mwaka huu inatarajiwa kufanyika December 3 mwaka huu, hukuj mji wa Limbe ukiwa ni mji mwingine mwenyeji.

Timu ya taifa ya Nigeria ndio bingwa mara nyingi zaidi wa soka la wanawake barani Afrika ambapo imeshawahi kulitwaa taji hili mara tisa, huku Equatorial Guinea likiwa ni taifa jingine ambalo limeshawahi kushinda taji hili.

Kundi A: Cameroon (wenyeji), Misri, Afrika Kusini na Zimbabwe.

Kundi B: Nigeria (mabingwa watetezi), Mali, Ghana na Kenya.

Nchi ya Kenya inashiriki kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya mwaka huu ambapo pia imefuzu kucheza hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Cecafa inayosimamiwa na baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati nchini Uganda.

Kenya itacheza na Tanzania kwenye fainali ya Cecafa upande wa wanawake siku ya Jumanne ya September 20, 2016.

Timu ya wanawake ya Ghana haijawahi kulitwaa taji hili kubwa barani Afrika upande wa wanawake, lakini imekuwa ikipoteza kwenye mchezo wa fainali kwa zaidi ya mara tatu, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1998, 2002 na mwaka 2006.

Timu ya taifa ya Mali ilitinga kwenye michuano ya mwaka huu, baada ya Equatorial Guinea kuondolewa kushiriki kutokana na kuchezesha mchezaji ambaye hakustahili.

Cameroon yenyewe itakuwa ikijaribu kutwaa tajik hili na kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya mwaka huu ukilinganisha na miaka miwili iliyopita ambapo walipoteza kwenye mchezo wa fainali nchini Namibia dhidi ya Nigeria.

Afrika Kusini na Zimbabwe zenyewe zitakuwa zinajaribu kuonesha misuli yao kufuatia ushiriki wa michezo ya Olimpiki ya Rio, ambapo kila timu iliaga michezo hiyo kwa kuambulia alama moja tu.

Misri mata ya mwisho kucheza michezo hii ilikuwa ni mwaka 1998 ambapo walipoteza kwenye mechi zao zote za kwenyeh hatua ya makundi na kukubali kubugizwa mabao 14.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.