Pata taarifa kuu
RIADHA-RIO

Mu Ethiopia Almaz Ayana aweka rekodi mpya ya dunia mita 10000

Mu Ethiopia, Almaz Ayana amefanikiwa kuweka rekodi ya dunia kwa upande wa wanawake katika mbio za mita elfu 10, baada ya kumaliza katika muda wa dakika 29 na sekunde 17, akivunja rekodi ya dunia ya awali iliyokuwa ya muda wa dakika 29 na sekunde 31.

Mwanariadha wa Ethiopia, Almaz Ayana akiwa kando ya bando linaloonesha muda aliomaliza kwenye fainali ya mbio za mita elfu 10 katika michezo ya Olimpiki ya Rio, Agosti 12, 2016
Mwanariadha wa Ethiopia, Almaz Ayana akiwa kando ya bando linaloonesha muda aliomaliza kwenye fainali ya mbio za mita elfu 10 katika michezo ya Olimpiki ya Rio, Agosti 12, 2016 REUTERS/Lucy Nicholson
Matangazo ya kibiashara

Ayana anaweka rekodi mpya ya dunia kwa mtindo wa aina yake akimpiku bingwa wa mbio hizo kwenye michezo ya Olimpiki ya London mwaka 2012, Tirunesh Dibaba aliyemaliza katika nafasi ya tatu.

Mkenya Alice Aprot Nawowuna ambaye ni mara yake ya kwanza kushiriki kwenye michezi ya Olimpiki inayofanyika jijini Rio, Brazil, alianza vema mbio hizo kwa kuwaacha wenzake, kabla ya kuishiwa pumzi wakati wa dakika za lala salama.

Mkenya mwingine, Vivian Cheruiyot, alimaliza kwenye nafasi ya pili kwenye mbio hizo kwa kutumia muda wa dakika 29 na sekunde 33, akishindwa kuitoa Kenya kimasomaso angalau kwa mara ya kwanza kutwaa medali ya Dhahabu.

Katika michezo ya Olimpiki, wanariadha wa Kenya hawajawahi kushinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita elfu 10, na walikuwa wakitarajia kufanya maajabu katika mbio hizi.

Hata hivyo wachambuzi wa michezo wanasema kuwa, ushindi wa wanariadha wa Kenya na hasa katika mbio za mita elfu 10, ni ushindi kwa bara la Afrika, na hii imeonesha nyota njema kwa wanariadha wengine wanaofuatia.

Wanariadha wengine waliofuatia kwenye mita elfu 10 ni pamoja na, Mkenya, Betsy Saina, Marekani, Molly Huddle, Yasemin Can kutoka Uturuki na Gelete Burka wa Norway.

Kwa matokeo haya, Ayana anajinyakulia medali ya dhahabu huku Mkenya, Cheruiyot akijinyakulia medali ya fedha na MuEthiopia Dibaba akijinyakulia medali ya Shaba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.