Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-RAGA

Timu ya taifa ya Kenya yaondoka mikono mitupu Brazil

Timu ya taifa ya mchezo wa raga ya Kenya yenye wachezaji saba kile upande, imeondoka katika michezo ya Olimpiki inayoendelea nchini Brazil  mikono mitupu baada ya kushindwa mechi zao zote katika hatua ya makundi.

Kikosi cha Kenya cha mchezo wa raga katika michezo iliyopita
Kikosi cha Kenya cha mchezo wa raga katika michezo iliyopita shujaapride.com
Matangazo ya kibiashara

Kenya ambayo ilikuwa katika kundi moja na Uingereza, Japan na New Zealand, ilimaliza ya mwisho baada ya kufungwa mechi zao zote.

Mchuano wa kwanza vijana hao kutoka Afrika Mashariki, walifungwa na Uingereza alama 31 kwa 7, wakalemewa na New Zealand alama 28 kwa 5 na mchuano wa mwisho walifungwa na Japan kwa alama 31 kwa 7.

Mbali na Kenya, mataifa mengine kama New Zealand, Ufaransa, Argentina na Australia yameyaaga mashindano haya baada ya kuondolewa katika hatua ya robo fainali.

Michezo ya nusu fainali inachezwa baadaye leo.

Nusu fainali ya kwanza itakuwa ni kati ya Fiji na Japan, huku Uingereza ikipambana na Afrika Kusini.

Fiji ilifuzu baada ya kuishinda New Zealand kwa alama 12 kwa 7, Japan nayo ikailemea Ufaransa pia kwa alama 12 kwa 7, Uingereza wakaingia baada ya kupata ushindi wa alama 5 kwa 0 dhidi ya Argentina huku wawakilishi wengine wa Afrika, Afrika Kusini wakiwalemea Australia alama 22 kwa 5.

Fainali ya kutafuta medali ya dhahabu itachezwa siku ya Ijumaa katika uwanja wa Deodoro jijini Rio de Janeiro.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.