Pata taarifa kuu
TENESI

Maria Sharapova asema ameonewa

Mchezaji tenesi mahiri na maarufu raia wa Urusi, Maria Sharapova, juma hili ameapa kukata rufaa dhidi ya adhabu ya kufungiwa kwa muda wa miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli.

Maria Sharapova
Maria Sharapova Jayne Kamin-Oncea-USA TODAY Sports TPX IMAGES OF THE DAY
Matangazo ya kibiashara

Adhabu hii dhidi ya Sharapova imetolewa baada ya wataalamu wa maabara na viongozi wa shirikisho la tenesi ITF kuridhia kutoa adhabu kwa mchezaji huyo aliyekiri kutumia dawa hizo kwa kile alichosema ni sababu za kiafya.

Sharapova mwenye umri wa miaka 29 hivi sasa, vipimo vyake vilionesha alitumia dawa zilizopigwa marufuku mchezoni wakati aliposhiriki mashindano ya Australian Open yaliyofanyika mwezi January mwaka huu.

Adhabu hii imemuweka pabaya mchezaji huyu ambaye ikiwa atashindwa kwenye rufaa yake, huenda akajikuta akilazimika kuachana na mchezo huo kwakuwa umri utakuwa umeenda wakati atakapomaliza adhabu yake.

Taarifa ya shirikisho la mchezo huo imesema kuwa "Tume huru iliyoundwa kufanya uchunguzi, ilibaini kuwa Sharapova alitenda kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli zinazokatazwa na hivyo alikiuka sheria hii, na hivyo ananyang'anywa ushindi wake na hatatakiwa kushiriki kwenye mashindano yoyote kwa muda wa miaka 2 kuanzia January 26 mwaka huu."

Akizungumzia adhabu aliyopewa, Sharapova amesema ni adhabu ambayo si ya haki kwakuwa tume ya awali iliweka wazi kuwa sikukiuka sheria yoyote, na kwamba hakubalini na adhabu hiyo.

Sharapova amelituhumu shirikisho la ITF kwa kutumia muda mwingi pamoja na raslimali nyingine ili kwa makusudi tu wamkute na hatia ya kukiuka sheria za matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku mchezoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.