Pata taarifa kuu
ITALIA-SOKA

McDonald Mariga achukuliwa adhabu

Mchezaji wa Kimataifa wa Kenya anayecheza soka la kulipwa katika ligi ya Serie B nchini Italia McDonald Mariga amefungiwa kutocheza michuano mitano baada ya kumsalimu kwa nguvu mwamuzi hadi akatoka damu mkononi.

Moja ya viwanja nchini Italia, ambapo McDonald Mariga amefungia michuano mitano kutokana na utovu wa nidhamu.
Moja ya viwanja nchini Italia, ambapo McDonald Mariga amefungia michuano mitano kutokana na utovu wa nidhamu. AFP PHOTO/NICHOLAS KAMM
Matangazo ya kibiashara

Mariga anayechezea klabu ya Latina aliondolewa uwanjani kipindi cha pili wakati wa mchuano na klabu ya Virtus Entella na kwenda kumpa mkono mwamuzi kabla ya kuondoka uwanjani.

Kiungo huyo wa kati aliyewahi kuichezea klabu ya Inter Milan, Parma, Real Sociedad na Helsingborgs IF amepatikana na kosa jingine la kumtupia maneno makali mwamuzi huyo.

Adhabu hii ya Kamati ya nidhamu inamaanisha kuwa Mariga mwenye umri wa miaka 29 hatoshiriki katika michuano inayosalia kabla ya msimu kumalizika.

Mariga alijiunga na klabu hiyo mwezi Januari na ameichezea mara 13 na kwa sababu ya adhabu hiyo atakosa mchuano muhimu dhidi ya Spezia siku ya Jumamosi.

Ni kaka yake Victor Wanyama anayechezea klabu ya Southmptom nchini Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.