Pata taarifa kuu
TENESI-UINGEREZA

Konta aingia kwenye orodha ya wachezaji 30 bora wa mchezo wa tenesi upande wa wanawake kwa mara ya kwanza

Siku chache baada ya kumalizika kwa michuano ya Australian Open, mcheza tenesi raia wa Uingereza, Johanna Konta amefanikiwa kutinga katika orodha ya 30 bora ya wachezaji wa tenesi upande wa wanawake.

Johanna Konta, mchezaji tenesi raia wa Uingereza
Johanna Konta, mchezaji tenesi raia wa Uingereza Reuterss/Issei Kato
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza kwa Konta kufika kweye nafasi za juu za orodha za wacheza tenesi kwa upande wa wanawake.

Konta alikuwa anashikilia nafasi ya 47 kabal aya orodha mpya kutolewa hapo jana, ambapo sasa amekwea hadi kwenye nafasi ya 28 katika orodha ya wachezaji bora wa tenesi kwa upande wa wanawake.

Angelique Kerber raia wa Ujerumani ambaye ni bingwa wa mwaka huu 2016 michuano ya Australian Openro Grand Slam de sua carreira.
Angelique Kerber raia wa Ujerumani ambaye ni bingwa wa mwaka huu 2016 michuano ya Australian Openro Grand Slam de sua carreira. REUTERS/Issei Kato

Konta amefikia nafasi hii baada ya kutinga kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya mwaka huu nchini Australia, na kufungwa kwenye hatua hiyo na mchezaji Angelique Kerber ambaye ndie bingwa wa michuano ya mwaka huu.

Kerber raia wa Ujerumani alifanikiwa kutwaa taji hili baada ya kumfunga mchezaji nambari moja kwenye orodha ya wachezaji tenesi kwa upande wa wanawake, Serena Williams raia wa Marekani.

Mchezaji mwingine wa Uingereza, Heather Watson baada ya kutolewa kwenye hatua ya kwanza kabisa ya michuano hii, ameporomoka kwa nafasi sita hadi kufikia nafasi ya 85.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.