Pata taarifa kuu
DRC-TP MAZEMBE-SOKA

TP Mazembe yaangukia pua kwa kufungwa mabao 2-1

Klabu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefungwa mabao 2 kwa 1 na Club ya America kutoka Mexico kuibuka katika nafasi ya tano katika mashindano ya dunia baina ya vlabu nchini Japan.

Wachezaji wa TP Mazembe kutoka DRC.
Wachezaji wa TP Mazembe kutoka DRC. Photo: TP Mazembe
Matangazo ya kibiashara

Mabao ya Club America yalitiwa kimyani na Dario Benedetto na mwezake Martin Zuniga katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo.

Bao la Benedetto lilitikisa nyavu za TP Mazembe katika dakika 19 ya mchuano huo, huku Zuniga akifunga la pili katika dakika ya 29, Mazembe nao walipata bao lao kupitia Rainford Kalaba katika dakika ya 43 ya kipindi hicho cha kwanza.

Baadhi ya mashabiki wanahisi kuwa maandalizi ya TP Mazembe hayakuwa mazuri kuelekea michuano hiyo huku wengine wakidokeza kuwa ilikuwa ni tu bahati mbaya kwa timu yao kufungwa.

Michuano ya nusu fainali ni siku ya Alhamisi, Barcelona watachuana na Guangzhou Evergrande ya China huku Sanfrecce Hiroshima ya Japan ikichuana na River Plate kutoka Argetina.

Watakaoibuka washindi watamenyana katika fanali siku ya Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.