Pata taarifa kuu
DRC-TP MAZEMBE-SOKA

Mashabiki wa TP Mazemba wapigwa na butwaa

Kumekuwa na hisia mseto nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya TP Mazembe kufungwa katika hatua ya robo fainali kuwania ubingwa wa kombe la dunia baina ya vlabu.

Timu ya TP Mazembe katika fainali ya Ligi ya Mabingwa nchini Algeria, Oktoba 31, 2015.
Timu ya TP Mazembe katika fainali ya Ligi ya Mabingwa nchini Algeria, Oktoba 31, 2015. AFP PHOTO / FAROUK BATICHE
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya mashabiki wanahisi kuwa maandalizi ya TP Mazembe hayakuwa mazuri kuelekea michuano hiyo huku wengine wakidokeza kuwa ilikuwa ni tu bahati mbaya kwa timu yao kufungwa.

Mchambuzi wa soka na mwandishi wa Habari wa AFP Lucien Kahozi Koshia ameiambia idhaa ya Kiswahili ya RFI akiwa mjini Osaka kuwa, wachezaji wa Mazembe walileemewa na kasi ya Sanfrecce Hiroshima.

Mazembe walionesha mchezo mzuri katika mechi zilizopita lakini pia katika mchuano wa robo fainali na licha ya kupata kona saba walishindwa kutumia nafasi hizo kupata ushindi.

“Wachezaji wa Mazembe wanaotoka nchi nane barani Afrika hawakuwa na mazoezi ya pamoja, hali ya hewa ilikuwa nzuri hapa Japan lakini Mazembe walielemewa”, amesema Kahozi.

Aidha, kwa mujibu wa Kahozi kutokuwepo kwa kipa wa siku nyingi na mwenye uzoefu mkubwa Robert Kidiaba, huenda kulichangia Mazembe kufungwa.

“Naamini kama Kidiaba angekuwa langoni, mambo yangekuwa tofauti. Kidiaba hapa Japan walikuwa wanamwogopa sana na hata nilishuhudia jezi yake ikiteketezwa moto”, ameongeza Kahozi.

TP Mazembe sasa itachuana na Cub ya America ya Mexico siku ya Jumatano kutafuta mshindi wa nafasi ya tano katika mashindano hayo.

Mapema siku ya Jumapili, Club America ilipoteza katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Guangzhou Evergrande ya China kwa mabao 2 kwa 1.

Michuano ya nusu fainali ni siku ya Alhamisi, Barcelona watachuana na Guangzhou Evergrande ya China huku Sanfrecce Hiroshima  ya  Japan ikichuana River Plate kutoka Argetina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.