Pata taarifa kuu
CONGO-MCHEZO-SOKA

Claude Le Roy ajiuzulu

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Congo Brazaville Mfaransa Claude Le Roy amejiuzulu.

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Congo Claude Le Roy (kulia) na Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Florent Ibenge.
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Congo Claude Le Roy (kulia) na Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Florent Ibenge. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya Le Roy, mwenye umri wa miaka 67, imekuja baada ya Congo kufuzu katika hatua ya makundi kuendelea kutafuta tiketi ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Kocha huyo amesema baada ya miaka miwili ya kuifunza Congo Brazavile ameona ni vema kuondoka kwenda kufanya kazi kwingineko.

Ripoti zinasema kuwa huenda akapewa kazi na Cameroon baada ya kocha wa timu hiyo ya taifa Volker Finke kujiuzulu.

Claude Le Roy amekuwa akifunza mataifa mbalimbali barani Afrika tangu mwaka 1985 alipoanza kuifunza Cameroon lakini pia amewahi kuifunza, Senegal, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na sasa Congo Brazaville.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.