Pata taarifa kuu
CAF-SOKA-AFRIKA

Mechi mbalimbali zapigwa mwishoni mwa juma hili

Michuano ya marudiano mzunguko wa tatu kufuzu katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika baina ya wachezaji wasiozidi miaka 23 inapigwa mwishoni mwa juma hili katika nchi mbalimbali barani Afrika.

Wakati mechi ya kufuzu ya AFCON 2015 kati ya Afrika Kusini na Sudan.
Wakati mechi ya kufuzu ya AFCON 2015 kati ya Afrika Kusini na Sudan. AFP PHOTO / EBRAHIM HAMID
Matangazo ya kibiashara

Uganda itamenyana na Misri Jumamosi hii jijini Kampala, na wana kazi kubwa baada ya kufungwa mabao 4 kwa 0 katika mchuano wa ugenini.

Vijana wa Uganda wanahitaji ushindi wa mabao 5 kwa 0 ili kufuzu katika fainali hizo zitakazopigwa nchini Senegal kati ya tarehe 28 mwezi Novemba hadi tarehe 12 Desemba.

Michuano hiyo pia itatumiwa kutafuta timu tatu za kwanza kufuzu katika michezo ya msimu joto ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mwaka ujao.

Mataifa manane yatashiriki katika michuano hii.

Michuano mingine ya kufuzu ni kati ya Congo Brazaville itakuwa nyumbani kumenyana na Nigeria, ambayo iliishinda mabao 2 kwa 1.

Gabon ambayo ilifungwa na Mali bao 1 kwa 0, itakuwa ugenini kumenyana na Mali katika uwanja wa Stade Modibo Keita jijini Bamako.

Mchuano mwingine mgumu siku ya Jumamosi ni kati ya Zambia na Cote d'Ivoire, baada ya mchuano wa kwanza kumalizika kwa sare ya kutofungana jijini Abidjan.

Vijana wa Afrika Kusini wapo nyumbani kuwakaribisha Zimbabwe baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1 kwa 1 katika mchuano wa kwanza.

Miamba wa soka Afrika Kaskazini Morocco na Tunisia nao watamenyana siku ya Jumapili baada ya Morocco kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0 katika mchuano wa mzunguko wa kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.