Fifa yatoa ripoti ya mwezi ya viwango vya soka dunia
Timu ya taifa ya Colombia imechukua nafasi ya tatu kulingana na ripoti iliyotolewa alhamisi wiki hii na shirikisho la soka duniani Fifa, baad ya kuipiku timu ya taifa ya Uholanzi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Katika ripoti hiyo ya Fifa, Ujerumani inaongoza ikifuatiwa na Argentina, huku Uholanzi ikichukua nafasi ya nne baada ya kufungwa na timu ya taifa ya Czech mabao (2-1).
Timu ya taifa ya Ubelgiji imechukua nafasi ya tano ikiwa mbele ya Brazili na Uruguay, ambyo imechukua nafasi ya 7.
Katika timu 10 bora, Brazil inachukua nafasi ya 6, Uhispania ikichukua nafasi ya 8, huku Ufaransa ikichukua nafasi ya 9 ikiwa mbele ya Uswisi.
Algeria ambayo ni moja ya mataifa ya Afrika yaliyoshiriki Kombe la dunia 2014, imechukua nafasi ya 20, ambapo Novemba mwaka 2012 ilichukua nafasi ya 19.
1. Ujerumani
2. Argentina
3. Colombia (+1)
4. Uholanzi (-1)
5. Ubelgiji
6. Brazil(+1)
7. Uruguay (-1)
8. Uhespania(-1)
9. Ufaransa(+1)
10. Uswiwi (-1)
11. Ureno
12. Chile
13. Italia (+1)
14. Ugiriki (-1)
15. Costa Rica
16. Mexico(+1)
17. Marekani (+1)
18. Uingereza(+2)
19. Croatia(-3)
20. Algeria (+4)
...