Pata taarifa kuu
UHISPANIA-REAL MADRID-Michezo

James Rodriguez anunuliwa na Real Madrid kwa kitita kikubwa

Mshambuliaji wa klabu ya As Monaco kutoka Colombia, James Rodriguez, mfungaji bora katika kombe la dunia, amesaini mkataba na klabu ya Real Madrid.

Wachezaji wa klabu ya Real Madrid.
Wachezaji wa klabu ya Real Madrid. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Klabu ya As Monaco imekubaliana na Real Madrid kumuuza mshambuliaji huyo wa kimataifa kitita cha Yuro kati ya milioni 75 na 80.

James Rodriguez, mwenye umri wa miaka 23, mfungaji bora katika kombe la dunia, ambaye aliifungia Colombia mabao 6, na kushindia tuzo ya Golden Boot, amekua anatarajiwa jumanne hii mchana kujiunga na klabu ya Real Madrid, kwa mujibu wa magazeti mawili ya michezo ya kila siku ya nchini Uhispania.

Hapo jumapili meneja mpya wa As Monaco, Leonardo Jardim, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Baranquilla nchini Colombia, alitupilia mbali madai hayo ya kuuzwa kwa James Rodriguez.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.