Pata taarifa kuu
CELTIC

Celtic yamtangaza Ronny Deila kuwa kocha wake mpya

Klabu ya Celtic nchini Scottland imemtangaza, Ronny Deila raia wa Norway kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa miezi 12 huku kukiwa na uwezekano wa mkataba huo kuongezwa. 

Kocha mpya wa Celtic, Ronny Deila
Kocha mpya wa Celtic, Ronny Deila Reuters
Matangazo ya kibiashara

Deila mwenye umri wa miaka 38 raia wa Norway anachukua jukumu la kuinoa timu hiyo toka kwa Neil Lennon ambaye aliachana na klabu hiyo punde baada ya kushinda taji la tatu mfululizo na timu hiyo.

Kocha huyu mpya ambaye amepata mafanikio kwenye klabu ya Norway ya Stronsgodset alifanikiwa kutwaa kombe la Tippeligaen na kombe la ligi kuu ya nchini Norway mwaka 2010.

Akizungumzia uteuzi wake, Deila anasema "Nitaheshimu nafasi hii niliyopewa na nitafanya kila linalowezekana kufikia mafanikio na malengo ya klabu ya Celtic". Alisema Deila.

Deila ameongeza kuwa "Ni jambo zuri kutangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu kubwa kama Celtic, moja ya klabu kubwa yenye mafanikio ya soka duniani na klabu ambayo nimekuwa nikiiheshimu". Alisema Deila.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.