Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-CAF-CHAN

Shirikisho la Soka barani Afrika latenga kitita chadola kwa mshindi wa michuano ya CHAN

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza kuwa mshindi wa michuano inayoendelea ya CHAN inayowahusisha wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani atapata kitita cha DOLA 750,000.

Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Issa Hayatou
Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Issa Hayatou RFI
Matangazo ya kibiashara

CAF pia imesema kuwa Dola Milioni 3 nukta 2 ziltagawanywa miongoni mwa timu zote 16 zilizoshiriki katika kinyanganyiro hicho.

Haya yanajiri, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Gabon zikijiunga na Mali, Nigeria, Morroco, Zimbabwe, Ghana na Libya katika hatua ya robo fainali.
Timu zote zilizokuwa zinawakilisha Afrika Mashariki zimeondolewa katika michuano hii, ikiwemo Uganda, Ethiopia na Burundi.

Katika michuano ya robo fainali zitakazopigwa mwishoni mwa juma hili, Morroco watapambana na Nigeria katika mchuano wa kwanza siku ya jumamosi, huku Mali wakimenyana na Zimbabwe.

Siku ya Jumapili, Gabon watamenyana na Libya, huku Ghana wakipangiwa kumaliza kazi na Jamhuri ya Kidemkorasia ya Congo.
Michuano ya robo fainali itachezwa siku ya Jumatano ijuma lijalo tarehe 29.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.