Pata taarifa kuu
UFARANSA

Timu vinara wa Soka nchini Ufaransa zashindwa kutamba kwenye mechi za ligi

Katika michuano ya ligi ya Ufaransa ambayo inaendelea, timu ya Paris SG imekwenda sare jana kwa kufungana na Lille mabao (2-2), huku Marseille ikifaulu kupanda ngazi kwa kutoka sare na Bordeaux kwa mabao (2-2). Paris SG haijafungwa toka mwezi wa novemba mwaka 2012.

KENZO TRIBOUILLARD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Paris SG inaongoza ikiwa na alama 44, ikiwa mbele ya Monaco ambayo ina alama 41, huku Lille ikiwa na alama 40.

Kabla ya mchuano wa marudio, Marseille ilikua iliifunga Bordeaux mabao 2-0, huku Lorient ikiwa mbele kwa mabao 2-0, ilitoka sare na Lyon kwa mabao 2-2.

Ni kwa mara ya pili katika michuano miwili ya Ligi kuu ya Ufaransa, kituko hicho kinatokea kwa timu ya Lyon, ambayo wiki iliyopita, ilikua ikiongoza kwa mabao 2-0 dhidi ya Marseille.

Kwenye uwanja wa Vélodrome, mashabiki wa Bordeaux walishangilia na kufurahia mabao yaliyowekwa wavuni na Romao pamoja na Gignac, katika dakika 73 na 74.

Hata hivo Bordeaux haijafanya vizuri, kwani inashikilia na fasi ya 4, nyuma ya Lille.

OM inachukua nafasi ya 6, ikishindwa alama 11 na Lille.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.