Pata taarifa kuu
UFILIPINO

Mwana masumbwi Manny Pacquiao kutembelea mji wa Tacloban baada ya ushindi

Mwana masumbwi Manny Pacquiao ameahidi kutembelea maeneo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino hasa kwenye mji wa Tacloban siku chache zijazo baada ya kutetea ubingwa wake.

bingwa wa ngumi Manny Pacquiao
bingwa wa ngumi Manny Pacquiao Mashindano ya kimataifa ya ngumi za uzani wa kati yametangazwa
Matangazo ya kibiashara

Mashindano ya kimataifa ya ngumi za uzani wa kati yametangazwa jana Jumapili kwenye vituo vinne vya wazi mjini Tacloban ili kuwatia moyo wakazi wa maeneo hayo baada ya kukumbwa na kimbunga kilichoathiri maisha yao.

Katika mashindano hayo mbunge Pacquiao akaibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake Brandon Rios kwa raundi 12 huko Maca ,na kutangaza kuwa kipaumbele chake ni kutembelea mji wa Tacloban kama alivyowaahidi wakazi wa mji huo.

Pacquiao ameongeza kuwa timu yake inashughulikia kupata taarifa zitakazo mwezesha kusafiri hadi kwenye mji mkuu wa jimbo la Leyte na atakuwa huko ndani ya siku chache zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.