Pata taarifa kuu
SOKA

Kocha mkuu wa timu ya soka ya Nigeria (U 17) asema hana hofu na Uswisi

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya vijana wa chini ya miaka 17 nchini Nigeria Manu Garba, ametangaza kuwa timu yake haina hofu na timu ya taifa ya Uswisi watakayo menyana nayo hii leo kwenye mchezo wa nusu fainali za kombe la dunia la chini ya miaka 17 mashindano yanayoendelea huko Dubai. 

Kocha mkuu wa timu ya Nigeria (U -17) Manu Garba
Kocha mkuu wa timu ya Nigeria (U -17) Manu Garba goal.com
Matangazo ya kibiashara

Timu ya Nigeria inakutana na Uswisi kwa mara ya pili katika mashindano hao baada ya kutoka sare ya magoli3-3 kwenye mzunguko wa kwanza ambapo kocha huyo anaamini kwamba vijana wake watafanya kazi nzuri safari hii bila hofu.

Garba amesema kuwa katika maisha yake hajawahi kuipa nafasi hofu na hajui hofu ni nini anachoamini ni kwamba lolote litakalotokea limepangwa na Mungu hivyo hana hofu na Uswisi

Aidha kocha huyo amesisitiza kuwa Kundi F katika mashindano hayo ndilo kundi imara baada ya kutoa timu tatu kati ya timu nne zilizofuzu kutinga katika hatua ya nusu fainali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.