Pata taarifa kuu
Ligi ya Mabingwa barani Ulaya

Arsenal yashindwa kutamba nyumbani chelsea yapeta AC Milan yalazimishwa sare, Olympique de Marseille yaangukia pua

Klabu ya Arsenal imeshindwa kutamba nyumbani mbele ya wajerumani Borusia Dortmund kwa kukubali kipigo cha mabao 2 kwa 1 ikiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, huku mshambuliaji wake Wilshare akipata jeraha na kutolewa nje ya uwanja.

mchezaji wa Arsenal Ozil kazini
mchezaji wa Arsenal Ozil kazini
Matangazo ya kibiashara

Borusia Dortmund ndio ilikuwa ya kwanza kuliona Lango la Arsenal kupitia mchezaji wake Henrikh Mkhitaryan kabla ya Olivier Giroud kusawazisha na kuwa 1-1.
Dakika 10 kabla ya kipenga cha mwisho, Arsenal walionekana kuzidiwa kasi na mshambuliaji Lewandowski ambaye alipachika bao la ushindi.

Katika mchezo mwingine, Chelsea imeshinda ugenini mabao 3-0 dhidi ya Schalke 04 ya Ujerumani, Fernando Torres alipachika mawili na Eden Hazard moja.

AC Milan ya Italia imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Barcelona katika mechi ya Ligi ya Mabingwa usiku wa jana katika Uwanja wa San Siro.
Mchezaji Robinho alitangulia kuwafungia wenyeji bao dakika ya tisa, baada ya kupewa pasi kutoka kwa Kaka- lakini Lionel Messi akaisawazishia Barca dakika ya 24 kwa pasi kutoka kwa Iniesta.

Mechi nyingine, Steaua Bucuresti imetoka 1 - 1 na Basel, Olympique de Marseille ikafungwa 2-1 na Napoli ya Italia, FC Porto imelala 1-0 mbele ya Zenit Petesbourg, Austria Wien imefungwa 3-0 na Atletico Madrid huku Celtic ikashinda 2 - 1 dhidi ya Ajax Amsterdam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.