Pata taarifa kuu
michezo

Lionel Messi kutinga kizimbani kesho Ijumaa kwa tuhuma za kukwepa kodi

Nyota wa mchezo wa soka na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani kwa mara nne mfululizo Lionel Messi anataraji kutinga kizimbani kesho Ijumaa kukabiliana na tuhuma za kukwepa kodi.

Mchezaji wa Barcelona Lionel Messi
Mchezaji wa Barcelona Lionel Messi REUTERS/Albert Gea
Matangazo ya kibiashara

Messi na baba yake Jorge Messi watafika mahakamani kesho Ijumaa asubuhi katika mji wa pwani wa Gava karibu na Barcelona ambako mchezaji huyo anaishi, akituhumiwa kukwepa kodi ya kiasi cha Euro milioni 4.16 kati ya mwaka 2006-2009.

Licha ya kuwepo kwa kesi hiyo mahakamani Messi hajaathiriwa kwa namna yoyote katika fani yake wakati nyota huyo wa Barcelona akifanikiwa kutikisa nyavu mara kumi katika mechi saba msimu huu na mabingwa hao wa Uhispania wakiendelea kutofungwa.

Kesi hiyo ilianza kuunguruma mahakamani mnamo mwezi June ambapo mwendesha mashataka alimtuhumu Messi kwa kukwepa kodi kwa kumilikisha haki za picha zake kwa kampuni binafsi.

Hata hivyo mwezi Julai Messi alisema kwamba hana hofu kama baba yake, anawaamini wanasheria wao kwamba watalishughulikia suala hilo na mambo yatakuwa sawa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.