Pata taarifa kuu
FIFA-QATAR 2022

Qatar yapinga pendekezo la michauno ya kombe la dunia mwaka 2022 kuhamishiwa nchi nyingine

Mkuu wa ujumbe wa nchi ya Qatar aliyefanikisha nchi hiyo kushinda tenda ya kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022, ametupilia mbali madai ya baadhi ya nchi kutaka michuano hiyo ihamishiwe taifa jingine.

Rais wa FIFA, Sepp Blatter akionesha bahasha iliyoipa ushindi nchi ya Qatar kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2022
Rais wa FIFA, Sepp Blatter akionesha bahasha iliyoipa ushindi nchi ya Qatar kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2022 Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa ujumbe wa Qatar, Hassan al-Thawadi ametupilia mbali madai ya nchi ya Uingereza kutaka michauno hiyo ihamishwe kwenda taifa jingine kutokana na hali ya hewa nchini Qatar kutoridhisha.

Uingereza pamoja na mataifa mengine ya bara la Ulaya wameonesha hofu yao kuhusu michuano hiyo kufanyika nchini Qatar kwa kile wanachodai kuwa ni kutokana na hali mbaya ya hewa ya joto ambayo inashuhudiwa nchini humo.

Hata hivyo hivi karibuni rais wa shirikisho la kabumbu duniani FIFA, Sepp Blatter alisema amewasilisha ombi maalumu kwa kamati ya utendaji ya FIFA kutaka michuano hiyo isogezwe mbele hadi kipindi cha baridi nchini humo.

Mwenyekiti wa chama cha soka nchini humo. Greg Dyke amekiri ombi hilo kuwasilishwa FIFA na kwamba kamati ya utendaji itakutana hivi karibuni kuangalia uwezekano wa kusogeza mbele tarehe ya kuanza kwa michuano hiyo.

Baadhi ya wajumbe walipendekeza michuano ya kombe la dunia nchini Qatar ifanyike wakati wa majura ya baridi na sio kipindi cha joto ambacho awali michuano hiyo ndio itatarajiwa kufanyika.

Mwezi June mwaka 2022 nyuzi joto nchini Qatar itafikia 50 hali ambayo kwa mataifa mengi yanaona kuwa itawaathiri wachezaji na hata mashabiki watakaoingia nchini humo kushuhudia michauno hiyo.

Qatar imesisitiza kuwa haoni haja kwanini michuano hiyo isifanyike nchini mwake wakati imetumia mabilioni ya fedha kuanza maandalizi ya kufanikisha fainali hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.