Pata taarifa kuu
SOKA

Super Eagles kutafuta ushindi muhimu kuelekea kufuzu kwa kombe la dunia

Timu ya taifa ya soka ya Nigeria itakuwa nchi ya kwanza kufuzu katika duru ya mwisho ya kusaka tiketi ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Brazil mwaka ujao ikiwa wataishinda Namibia leo Jumatano jijini Windhoek.

Matangazo ya kibiashara

Nigeria wanaongoza kundi la F kwa alama 8, watakuwa na alama 12 ikiwa watapata ushindi huo na kuomba kuwa Malawi wasishinde mchuano wake.

Malawi ambayo ni ya pili kwa alama 6 watamenyana na Harambee Stars ya Kenya jijini Blatyre wiki moja baada ya kutofungana na Namibia.

Kocha wa Super Eagles Stephen Keshi, amesema kuwa atatumia mfumo wa 4-3-3 dhidi ya Namibia mfumo ambao amesema ulifanya kazi wakati wa mchuano wao na Kenya na kufanikiwa kupata ushindi wa bao moja kwa 1 jijini Nairobi.

Namibia ambao ni wa tatu katika kundi hilo kwa alama nne wamepoteza matumaini ya kusonga mbele na kufuzu kwenda Brazil na watacheza mchuano wa leo bila ya kocha wake Roger Palmgren ambaye alijiuzulu siku ya Jumatatu kwa madai kuwa anahofia usalama wake.

Baada ya kuondoka nchini Namibia, Super Eagles wataelekea nchini Brazil kuungana na mataifa ya Uhispania kutoka barani Ulaya, Japan kutoka barani Asia, Mexico, Uruaguay, Tahiti na Italia kushiriki katika mashindano ya Mashirikisho.

Kutakuwa na makundi mawili katika kinya'nga' nyiro na kundi la kwanza kutakuwa na Brazil, Japan, Mexico na Italia, huku kundi la pili likiwa na Uhispania ,Uruguya, Tahiti na Nigeria.

Mchuano wa ufunguzi Jumamosi hii utakuwa kati ya wenyeji na mabingwa watetezi Brazil na Japan huku wawakilishi wa Afrika Nigeria wakicheza mchuano wao wa ufunguzi dhidi ya Tahiti siku ya Jumatatu ijayo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.