Pata taarifa kuu
SOKA-UHISPANIA

Klabu ya Real Madrid yasema Zinedine Zidane hana uzoefu wa kutosha kupewa jukumu la kuifundisha timu hiyo

Klabu ya Real Madrid imekiri Kungo wake za zamani raia wa Ufaransa Zinedine Zidane amefuzu kwa kiwango kinachotakiwa kwenye mafunzo yake ya ukocha lakini hawezi akapewa jukumu la kuinoa timu hiyo kwa sasa. Rais wa Real Madrid Florentino Perez amesema wanatambua uwezo wa Zinade lakini kwa sasa wanahitaji kocha ambaye ana ujuzi mkubwa zaidi ambao kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa hajaufikia.

Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ufaransa Zinedine Zidane ambaye kukosa kwake uzoefu kumemfanya ashindwe kupewa kazi ya kuinoa Real Madrid
Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ufaransa Zinedine Zidane ambaye kukosa kwake uzoefu kumemfanya ashindwe kupewa kazi ya kuinoa Real Madrid ikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Perez amesema timu hiyo itatafuta mtu mwingine ambaye atakuwa mrithi wa Jose Mourinho waliyekubaliana naye kusitisha mkataba naye lakini hatokuwa Zidane kama ambavyo ilikuwa inatajwa.

Rais huyo wa Klabu ya Real Madrid amesema kwa sasa wanahitaji kuwa makini kupata Kocha ambaye atahakikisha umaarufu wao ulioanza kupotea unarejea tena kwa hiyo watamtafuta Kocha mzoefu.

Perez amesema wanatambua uwezo na wanaheshimu sana kile ambacho kinafanywa na Zidane katika benchi la ufundi lakini wanatambua muda wa yeye kukabidhia jukumu la kuinoa timu hiyo akiwa Kocha Mkuu bado haujafika.

Kiongozi huyo wa Real Madrid amesisitiza Zidane ataendelea kuongoza mipango aliyopewa ikiwemo kusaka vipaji kwa ajili ya kujenga timu bora zaidi katika siku za usoni na kumshauri Kocha Mkuu atakayetangazwa.

Perez pia amekanusha madai ya wao kutaka kumchukua Kocha wa Paris Saint-Germain Carlo Ancelotti akisema wao wanatambua kwa sasa bado ana mkataba na mabingwa hao wa Ufaransa.

Klabu ya Real Madrid imesema yenye imekuwa katika urafiki wa karibu na PSG hivyo haipo tayari kuingia kwenye mgogoro na timu hiyo na kwa sasa wanaendelea kufanya mchakto wa kupata mrithi sahihi wa Mourinho aliyerejea Chelsea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.