Pata taarifa kuu
TENNIS-FRENCH OPEN

Serena Williams afanikiwa kutinga Robo Fainali ya French Open kwa kumfunga Roberta Vinci

Mchezaji Tennis anayeorodheshwa katika nafasi ya kwanza kwa ubora wa Tennis Duniani upande wa Wanawake Serena Williams amefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya mashindano ya French Open. Serena amefuzu kutinga hatua ya Robo Fainali baada ya kumfunga Roberta Vinci kutoka Italia kwa kumchakaza kwa seti mbili bila ya jibu kwa kushinda kwa 6-1 na 6-3 na kuendelea kuwinda taji hilo kwa mara nyingine.

Mchezaji nambari moja Upande wa Wanawake Duniani Serena Williams akirudisha mpira kwenye mchezo dhidi ya Roberta Vinci
Mchezaji nambari moja Upande wa Wanawake Duniani Serena Williams akirudisha mpira kwenye mchezo dhidi ya Roberta Vinci
Matangazo ya kibiashara

Mwanadada huyo katika Mashindano ya French Open hadi kufika sasa hajafungwa hata seti moja huku michezo yake yote akishindwa kwa seti mbili bila ya majibu dhidi ya wapinzani wake.

Baada ya Mchezo huo Serena alikiri Mpinzani wake Vinci alikuwa anatoa upinzani wa hali ya juu kwenye mchezo wao licha ya kumshinda kwa seti hizo mbili bila lakini mchezo ulikuwa mgumu.

Serena ameendelea kusisitiza kuwa lengo lake ni kutwa taji la French Open kwa mwaka huuna hatua yake ya kutinga Robo Fainali imekuwa chachu tu ya kumfanya aendelee kusonga mbele na hatimaye kutimiza ndoto zake.

Michezo mingine imeshuhudia Svetlana Kuznetsova akitinga Robo Fainali baada ya kumfunga Angelique Kerber kwa jumla ya seti mbili kwa moja kwa matokeo ya 6-4, 4-6 na 6-3.

Carla Suarez Navarro ameshindwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya French Open baada ya kufungwa na Sara Errani kwenye mzunguko wa nne baada ya kufungwa kwa seti mbili kwa moja kwa matokeo ya 5-7, 6-4 na 6-3.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.