Pata taarifa kuu
SOKA

Morroco na Tunisia zafuzu nusu fainali michuano ya soka baina ya chipukizi barani Afrika

Timu za taifa za soka ya Morroco na Tunisia zimefuzu katika nusu fainali ya mchuano wa kuwania ubingwa wa Afrika baina ya wachezaji wasiozidi miaka 17 na watacheza siku ya Ijumaa kuamua kiongozi wa kundi la A.

Matangazo ya kibiashara

Wenyeji Morroco walifuzu baada ya kuishinda Botswana mabao 3 kwa 0 na mchuano mwingine utakaoachezwa Ijumaa utakuwa kati ya Bostwana na Gabon ambao tayari wameondolewa katika mashindnao hayo.

Carthage Eaglets ya Tunisia walikuwa wa kwanza kufuzu nusu fainali hiyo baada ya kuishinda Gabon mabao 4 kwa 2 mjini Casablanca.

Nigeria ambayo ilianza mashindano hayo kwa ushindi wa mabao 6 jwa 1 dhidi ya Ghana, inamenyana na Cote Dvoire siku ya Jumatano kutafuta nafasi ya kufuzu kwa nusu fainali ya michuano hiyo.

Timu zingine zinazochuana katika kundi hilo ni kati ya Congo na Ghana.

Kocha wa Ghana Samuel Kwesi Fabin amekiri kuwa kufungwa na Nigeria ilikuwa ni kwa sababu ya kutumia mbinu zisizofaa katika mchuano huo.

Burkina Faso ilinyakuwa ushindi wa makala yaliyopita yalioandaliwa jijini Kigali Rwanda mwaka 2011 baada ya kuwashinda wenyeji kwa mabao 2 kwa 1 katika uwanjan wa Amahoro.

Timu zote nne zitakazofika katika awamu ya nusu fainali zitaliwakilisha bara la Afrika katika mashindano ya kombe la dunia yatakayofanyika katika Mmiliki za kiarabu kati ya tarehe 17 hadi tarehe 8 mwezi Novemba mwaka huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.