Pata taarifa kuu
SOKA-ULAYA

Lazio na Fiorentina zatinga robo fainali kombe la Italia

Mechi za makundi katika michuano ya kombe la soka nchini Italia zimeendelea kutimua vumbi hapo jana ambapo timu ya Lazio na Fiorentina zimefanikiwa kuingia kwenye robo fainali ya Kombe hilo. 

Nembo za timu za Lazio na Fiorentina  za Italia
Nembo za timu za Lazio na Fiorentina za Italia mcalcio.com
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kumalizika kwa mtanange uliolazimisha sare ya goli moja kati ya Lazio Rome na Siena na kufuatiwa na mikwaju ya penalti,hatimaye Lazio ikicheza nyumbani, imeichapa Siena kwa magoli manne.

Wakati huohuo, timu ya Fiorentina meishinda Udinese kwa goli moja kwa bila kwa jitihada za mchezaji wa kimataifa mwenye asili ya Uhispania Borja Valero dakika ya 36.

Katika mechi nyingine timu ya Bologna imeichapa timu ya Naples kwa magoli mawili kwa moja, goli la ushindi likifungwa katika dakika za majeruhi, na mchezaji kiungo mwenye asili ya Ugiriki Panagiotis Kone dakika ya tisini na moja.

Michuano ya Robo fainali katika kutafuta mshindi wa kombe la italia inatarajiwa kufanyika tarehe tisa januari mwakani ambapo Inter Milan itapambana na Bologne, AS Rome itakutana na Fiorentina, Lazio itachuana na Catane na AC Milan itamenyana na Juventus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.