Pata taarifa kuu
TENNIS

Novak Djokovic na Serena Williams ndio wachezaji bora wa Tennis mwaka 2012

Wachezaji wa kimataifa wa mchezo wa Tennis, Novak Djokovic kutoka Serbia na Serena Williams kutoka Marekani ndio wachezaji bora wa mchezo huo mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wamepata tuzo hizo kutoka kwa shirikisho la kimataifa cha mchezo wa Tennis ITF kutokana na umahiri na jitihada zao katika michuano mbalimbali mwaka 2012.

Novak Djokovic mwenye umri wa miaka 25 mbali na kupata tuzo la mchezaji bora mwaka huu pia atakumbukwa mwaka 2012 kwa kuorodheswa kuwa mchezaji bora wa kiume duniani baada ya kufanikiwa kushinda mataji ya Australian Open na kufika fainali  ya US Open.

Serena Willlims naye mwenye umri wa miaka 31 atakumbukwa mwaka huu kwa kushinda mataji ya Wimbledon na US Open kwa upande wa akina dada na kumaliza wa kwanza kwa upande wa akina dada.

Aidha, shirikisho hilo limewatangaza Bob na Mike Bryan ambao ni kaka wa toka nitoke raia wa Marekani kuwa washindi wa mwaka huu wachezaji bora wa mwaka katika kitengo cha kucheza wachezaji wawili wawili.

Bob na Mike wameshinda mashindano ya kimataifa mara tisa kati ya kumi ambayo wameshiriki pamoja.

Tuzo kwa upande wa akina dada ilimwendea Sara Errani na Roberta Vinci kutoka Italia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.