Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Man City yatimba kileleni baada ya kuichapa Aston Villa 5-0

Timu ya Manchester City imefanikiwa kukaa kileleni katika michuano inayoendelea ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kuichakaza timu ya Aston Villa kwa mabao matano kwa nunge katika mtanange wa jana Jumamosi huku timu za Manchester United na Chelsea zikikosa ushindi katika mechi zao. 

David Silva akifurahia baada ya kuifungia Man City bao la kwanza
David Silva akifurahia baada ya kuifungia Man City bao la kwanza telegraph.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Timu ya Man u ilikubali kichapo cha goli moja bila majibu kutoka kwa Norwich City , hivyo kuifanya timu hiyo ishindwe kufurukuta , huku Chelsea ambayo inashika nafasi ya sasa katika msimamo wa ligi hiyo tayari imecheza michezo minne bila kupata ushindi baada ya kufungwa magoli mawili kwa moja na West Bromwich Albion.

Goli la David Silva katika dakika ya 43 ya mchezo. Ndilo lililoiweka Man City kileleni katika mtanange uliopigwa kwenye dimba la Etihad, kabla ya mikwaju ya penati kutoka kwa Sergio Aguero na Carlos Tevez baada ya Andreas Weimann na Barry Bannan kuunawa mpira.

Katika dakika ya 67 ya mchezo Aguero alicheka na nyavu za Villa kwa mara nyingine tena baada ya mlinda mlango Brad Guzan kushindwa kuhimili shuti kali lililogonga posti na kisha kuzama kimiani na kisha Tevez kukamilisha idadi ya magoli matano.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.