Pata taarifa kuu
Uswisi

Kiongozi wa zamani wa Shirho la Soka Barani Asia Mohamed bin Hammam aongezewa adhabu ya kifungo cha kutojishirikisha na shughuli za Soka

Shirikisho la Soka duniani, FIFA limeongeza Muda wa adhabu wa Mgombea wa zamani wa Shirikisho hilo Mohamed Bin Hammam kwa siku nyingine 45, shirikisho hilo limeeleza katika Taarifa yake.

Kiongozi wa zamani katika Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Asia Mohamed Bin Hammam
Kiongozi wa zamani katika Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Asia Mohamed Bin Hammam
Matangazo ya kibiashara

Bin Hammam alipewa adhabu ya kufungiwa maisha kujishughulisha na Soka, hukumu ambayo litenguliwa na Mahakama ya Upatanishi ya Michezo, CAS mwezi Julai na kisha akapewa adhabu ya utojishughulisha na soka kwa siku 90.
 

hivi sasa Hammam aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Asia na aliyekuwa Mpinzani wa Sepp Blatter wakati wa kinyang'anyiro ch kuwania Urais wa FIFA amepatiwa adhabu zaidi ya kufungiwa.
 

Hatua hiyo imeelezwa na Wakili wa Bin Hammam kuwa ya kushangaza na kusema kuwa FIFA imeshindwa kutoa sababu za kuongezwa Muda wa adhabu hiyo.
 

Bin Hammam alishutumiwa kujaribu kununua Kura za maafisa wa Karibea kwa kuwapatia kitita cha Dola za kimarekani 40,000 kila mmoja ili kuwa Rais wa FIFA.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.