Pata taarifa kuu
Uswisi

Teknolojia mpya ya kubaini Kama Mpira umevuka Mstari wa golini au la kuanza kutumika

Wasambazaji wa Teknolojia ya kutambua iwapo mpira umevuka mstari wa golini au la katika mchezo wa mpira wa Miguu ya Goal Ref na Hawk-Eye wamepewa idhini ya kuweka mtandao wao dunia nzima baada ya kutia saini leseni ya Makubaliano na Shirikisho la Soka duniani, FIFA.Shirikisho hilo limeeleza hii leo.

Rais wa Shirikisho la Soka duniani,FIFA,  Sepp Blatter
Rais wa Shirikisho la Soka duniani,FIFA, Sepp Blatter REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limekuja ikiwa ni mwaka mmoja baada ya FIFA kuwa katika hatihati za kusaka Chombo hicho kitakachoweza kubaini kama Mpira umevuka Mstari wa Golini au la.
 

Taarifa ya FIFA imesema kuwa kati ya mwezi Oktoba mwaka 2011 na Mwezi Julai mwaka huu kampuni hizo zimekuwa zikifanya Majaribio madhubuti ya katika Maabara na katika viwanja nyakati za Mechi za moja kwa moja.
 

Bodi ya Shirikisho la kimataifa la mpira wa Miguu, IFAB, liliridhia matumizi ya Teknolojia hiyo Mwezi July kufuatia kuwepo kwa Mfululizo wa Matukio ambayo Waamuzi wamekuwa wakishindwa kuona kama Mpira umevuka Mstari wa Goli au la.
 

FIFA imesema kuwa Teknolojia hizo zinatakiwa kuonesha mafanikio makubwa viwanjani kabla ya kuanza kutumika rasmi duniani kote.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.