Pata taarifa kuu
Michezo-Football

Ligi kuu barani Ulaya kutimua vumbi mwishoni mwa Juma hili

Ligi kuu barani Ulaya za timuwa vumbi mwishoni mwa juma hili. Nchini Ujerumani ni wiki ya Nane leo Ijumaa Octoba 19 ambapo timu za Hoffenheim-Greuther Fürth zinashuka dimbani huku kesho jumamosi Octoba 20 Borussia-Schalke 04, Fortuna Dusseldorf-Bayern Munich Francfort-Hanovre Leverkusen-Mayence Wolfsburg-Fribourg zitakuwa uwanjani kumenyana na saa kumo na mbili nanusu Werder Brême-M'Gladbach zitakuwa uwanjani zikitimua vumbi. Siku ya jumapili Octoba 21 saa tisa na nusu Nuremberg-Augsburg.

Andrea Pirlo, wa Juventus (g.) na Stevan Jovetic wa Fiorentina (d.),
Andrea Pirlo, wa Juventus (g.) na Stevan Jovetic wa Fiorentina (d.), REUTERS/Giampiero Sposito
Matangazo ya kibiashara

Nchini Uingereza hii ni wiki ya saba Jumamosi Octoba 20 saa saba na dakika 45 Tottenham itachuana naChelsea wakati saa kumi kamili Fulham- ikijipima nguvu na Aston Villa na wakati huo huo Liverpool itapakuwa ikipambana na Reading, Manchester United itakutana na Stoke City, Swansea na Wigan, West Bromwich na Manchester City, West Ham itakutana na Southampton, saa kumi na mbili jioni Norwich itakuwa uwanjani kumeyana naArsenal

Na huki Ubelgini ikiwa katika wiki ya kumi na moja Anderlecht wanakutana jioni hii na Waasland Beveren na hapo kesho Jumamosi Genk wanakutana na Anvers wakati Cercles Bruges ikikutana na Malines huku La Gantoise wakipimana na Courtrai

Nchini Uhispania wakiwa katika wiki ya Nane kesho Jumamosi Malaga itakuwa uwanjani kumenyana na Valladolid wakati saa kumi na mbili jioni Real Madrid ikikwaruzana na Celta Vigo nayo Valence itapambana na Athletic Bilbao. Saa nne usiku Barcelona wataskuwa na La Corogne

Ligi kuu nchini Italia ipo katika wiki ya nane, Juventus itapambana na Naples huku Lazio Rome ikikwaruzana na AC Milan. Jumapili Octoba 21 Cagliari watakuwa uwanjani kumenyana na Bologne huku Atalanta ikipambana na Sienne

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.