Pata taarifa kuu
soka

Barcelona, Chelsea na Manchester United kutafuta ushindi mechi za UEFA

Mechi kadhaa za mkondo wa pili za mchezo wa soka kuwania taji la klabu bora barani Ulaya zinachezwa Jumanne usiku.

Matangazo ya kibiashara

Mabingwa wa zamani Barcelona watakuwa ugenini dhidi ya Benfica ya Ureno mchuano ambao kocha wa Barcelona Tito Vilanova amesema haamini utabiri wa kocha wa Benfica Jorge Jesus kuwa mchuano huo utamalizika kwa sare ya kutofungana.

Katika historia ya vlabu hivi viwili, Barcelona ilitoka sare ya kutofungana na Benfica mwaka 2006 na 1991 jijini Lisbon.

Banfica haijawahi kuifunga timu yeyote kutoka Uhispania kwa kipindi cha miaka 30, na mara ya mwisho kwa timu hizi mbili kukutana ilikuwa mwaka 2011 ambapo Barcelona iliishinda kwa mabao 2 kwa 0 na  kunyakua taji la UEFA Super Cup.

Barcelona na Benfica zinaanza kampeni za kuwania taji hilo huku zikiwa hazijapoteza mchuano wowote katika ligi ya soka katika mataifa yao.

Mchuano mwingine ambao pia unathathminiwa na mashabiki wa soka ni kati ya klabu ya Uingereza Manchester United na CFR Cluj ya Romania timu ambayo wengi hawaipi nafasi kubwa ya  kusonga mbele katika michuano ya UEFA.

Kocha wa Manchester City Sir Alex Ferguson amesema kuwa ni sharti wachezaji wake waiheshimu klabu hiyo na kuwataka kuwa makini na safu yao ya ushambuliaji kwani inaweza kufunga bao la mapema na kushinda mchuano huo .

Mabingwa watetezi Chelsea pia kutoka Uingereza watacheza na Nordsjaelland ya Denmark wakiwa na rekodi nzuri ya kutoshindwa na klabu yeyote kutoka nchini humo.

Chelsea ambayo ilianza kampeni ya kuetetea taji hili ilitoka sare ya mabao 2 kwa 2 katika mchuano wake wa ufunguzi dhidi ya Juventus ya Italia.

Mechi zingine zitakazochezwa ni pamoja na BATE dhidi ya Bayern Munich na Valencia na  Lile.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.