Pata taarifa kuu
UHISPANIA-UINGEREZA-UFARANSA-UJERUMANI

Real Madrid na Arsenal wachomoza na ushindi kwenye michezo yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya

Goli la dakika za lala salama lililopachikwa kimiani na Cristiano Ronaldo lilipeleka ushindi kwa Klabu ya Real Madrid kwenye mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Manchester City ambao ulimalizika kwa matokeo ya magoli 3-2.

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo akishangilia goli lake kwenye mchezo dhidi ya Manchester City
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo akishangilia goli lake kwenye mchezo dhidi ya Manchester City
Matangazo ya kibiashara

Manchester City walifanikiwa kuongoza mara mbili tofauti kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu kwa magoli ya kwake Edin Dzeko na Alexsandar Kolarov lakini Real Madrid walifanikiwa kusawazisha.

Dakika nne kabla ya mchezo kumalizika Real Madrid walikuwa nyuma kwa magoli 2-1 kabla ya Karim Benzema na Cristiano Ronaldo hawajafunga na kuipa ushindi wake wa kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi.

Kocha wa Real Madird Jose Mourinho amesema timu yake imepoteza kujiamini na wasingeweza kucheza zaidi ya walivyofanya huko Roberto Mancini akisema hakuna mtu anayepaswa kumlaumu mwezie.

Arsenal wakicheza ugenini nchini Ufaransa wakafanikiwa kuchomoza na ushindi wa magoli 2-1 mbele ya mwenyeji wao Montpellier ambao walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia Younes Belhanda.

Lakini magoli ya kwake Lukas Podolski na Gervinho yakatosha kupeleka ushindi kwa kikosi hicho ambacho kinanolewa na Arsene Wenger ambaye ameridhishwa na namna ambavyo timu yake imecheza.

Borussia Dortmund wakiwa nyumbani wakachomoza na ushindi mwembamba wa goli 1-0 mbele ya Ajax Amsterdam kupitia goli la Robert Lewandowski wakati AC Milan ikishindwa kutamba nyumbani na kutoa sare ya bila kufungana na Anderlecht.

FC Porto wakaibuka na ushindi mbele ya Dinamo Zagreb kwa magoli 2-0 wakati PSG wenyewe wakichomoza na ushindi mnono wa magoli 4-1 dhidi ya Dynamo Kiev.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.