Pata taarifa kuu
Qatar

Shirikisho la Soka Barani Asia kufanya Uchunguzi dhidi ya aliyekuwa Kiongozi wa Shirikisho hilo

Shirikisho la Soka barani Asia (AFC) linaendelea na Uchunguzi wake katika kashfa iliyomhusisha Rais wa Shirikisho hilo Mohamed Bin Hammam mbali na Adhabu yake kumalizika siku ya jana.

Kiongozi wa zamani katika Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Asia Mohamed Bin Hammam
Kiongozi wa zamani katika Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Asia Mohamed Bin Hammam REUTERS
Matangazo ya kibiashara

AFC inafanya Uchunguzi Madai ya Matumizi mabaya ya Fedha yanayoelezwa kufanywa na Bin Hammam wakati akiwa Kiongozi wa Shirikisho hilo.

Shirikisho hilo lililoongozwa na Hamman kwa takriban Muongo mmoja, lilimsimamisha Raia huyu wa Qatari kwa siku 30 tarehe 16 Mwezi Julai kisha kubadili kipengele cha Sheria kilichowaruhusu kuongeza adhabu kwa siku 20 zaidi Mwezi uliopita.

Mbali na kuisha kwa adhabu,Hammam 63 anaendelea kuwa katika adhabu ya kutojihusisha na shughuli zozote zihusuzo Soka kutokana na adhabu ya siku 90 iliyotolewa na FIFA tarehe 26 Mwezi Julai, AFC imeeleza kwenye Taarifa yake hii leo.
 

FIFA iliwahi kumuadhibu kifungo cha Maisha kushiriki shughuli za Soka kutokana na shutma za rushwa wakati akiwania kuwa Rais wa FIFA Mwaka jana lakini Mahakama inayoshughulikia Migogoro ya Michezo, CAS ikatengua Adhabu hiyo Tarehe 19 mwezi Julai.

Bin Hamman amekana Shutma zilizotolewa na AFC na FIFA na kusema kuwa atachukua hatua zaidi kuthibitisha kuwa hana hatia.
 

Zhang Jilong amekuwa akiongoza AFC wakati huu ambapo Hammam akitumikia adhabu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.