Pata taarifa kuu
SOKA-ULAYA

Msimu wa soka kuanza barani Ulaya

Msimu wa soka barani Ulaya unaanza mwishoni mwa wiki hii baada ya mapumziko ya miezi kadhaa na usajili wa wachezaji kukumamilika.

Matangazo ya kibiashara

Ligi ya Uingereza inayofuatwa zaidi na wapenzi wa soka katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati inaanza Jumamosi hii huku mechi kadhaa zikiratibiwa kuchezwa.

Kikubwa ambacho kimeendelea kuzungumziwa nchini Uingereza ni usajili mkubwa kuwahi kufanyika katika historia ya klabu ya Manchster United na Arsenal, baada ya Arsenal kumuuza nahodha wake Robin Van Persie kwa kima cha Pauni Milioni 24.

Arsenal ambayo imempoteza mshambulizi huyo aliyekuwa anategemewa sana katika klabu hiyo katika safu ya ufungaji mabao, watafungua mchuano wao dhidi ya Sunderland, Newcastle wacheze na Tottenham Hostpurs huku West Ham ikimenyana na Aston Villa.

Robin Van Persie anatarajiwa kuichezea Manchester United kwa mara ya kwanza siku ya Jumatatu dhidi ya Everton na kuongoza safu ya mashambulizi pamoja na Wayne Rooney.

Nchini Uhispania ,Lionel Messi wa Barcelona anasema msimu wa mwaka huu hautakuwa ni kutafuta bingwa kati yake na Christiano Ronaldo wa RealMadrid, bali utakuwa ni msimu wa kusaka bingwa wa taji  la La Liga kati ya Barcelona na Real Madrid.

Ligi ya Ufaransa ilianza Ijumaa mchuano wa ufunguzi kati ya Lille na AS Nancy.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.