Pata taarifa kuu
LONDON OLIMPIKI 2012

Rais Jonathan akasirishwa na matokeo mabaya ya Nigeria katika michezo ya Olimpiki

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameamuru mabadiliko katika uongozi wa michezo nchini humo baada ya nchi hiyo kushindwa kupata hata medali moja katika michezo iliyomalizika ya Olimpiki jijini London nchini Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Hii ndio mara ya kwanza kwa Nigeria kurudi nyumbani mikono mitupu ndani ya miaka 20,likiwa taifa ambalo limekuwa likishinda medali mbalimbali katika mbio fupi ,mchezo wa ndondi na soka.

Waziri wa Michezo nchini humo Labaran Maku amesema kuwa rais Jonathan ameamuru uongozi wa sekta mbalimbali za michezo kubadilisha uongozi wake uamuzi uliofikiwa jana katika baraza la Mawaziri.

Rais Jonathan atakumbukwa mwaka 2010 kutangaza kuivunjilia mbali timu ya taifa ya soka Super Eagles baada ya kutofanya vizuri katika mashindano ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini na pia kushindwa kufuzu kwa mechi za kutafuta bingwa wa Afrika mapema mwaka huu.

Mataifa mengi ya Afrika kama Kenya imekuwa ikishtumiwa na wapenzi wa michezo kwa kutofanya vema katika michezo ya Olimpiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.