Pata taarifa kuu
CECAFA

Yanga yaishinda APR 2-0 michuano ya CECAFA

Mabingwa watetezi wa taji la klabu bora Afrika Mashariki na Kati Yanga ya Tanzania wameifunga APR ya Rwanda kwa mabao 2 kwa 0 katika mchuano wa kutamatisha mechi za kundi la tatu katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Yanga walitawala mchuano huo licha ya kupata ushindani mkali kutoka kwa APR hasa katika kipindi cha pili cha mchuano huo kwa kukosa nafasi nyingi za kupata bao.

Tayari Yanga na APR zimefuzu katika hatua ya robo fainali pamoja na Atletico ya Burundi.

Katika mchuano mwingine URA ya Uganda iliishinda AS Ports ya Djibouti mabao 3 kwa 1 katika mchuano wao wa mwisho wa kundi la kwanza.

Vijana wa Ports wanarudi nyumbani baada ya kupoteza mechi zao zote dhidi ya Simba ya Tanzania na Vita Club ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Jumamosi Tusker ya Kenya iliyotoka sare ya kutofungana na Mafunzo ya Zanzibar inacheza mechi yake ya mwisho ya kundi la pili ya Azam FC ya Tanzania mchuano ambao ni sharti washinde ili kusonga mbele.

Simba ya Tanzania itamenyana na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchuano wa kumaliza ratiba ya kundi lao.

Jumapili ni siku ya mapumziko kabla ya robo fainali kuchezwa siku ya Jumatatu juma lijalo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.