Pata taarifa kuu
UHISPANIA-ITALIA-UKRAINE

Uhispania Mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya 2012 kwa kuifunga Italia kwenye Fainali

Timu ya Taifa ya Uhispania imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya ya mwaka 2012 baada ya kuishushia kichapo kizito timu ya taifa ya Italia kwenye mchezo wa fainali uliopigwa nchini Ukraine.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Uhispania wakishangilia Ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya wa mwaka 2012
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Uhispania wakishangilia Ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya wa mwaka 2012
Matangazo ya kibiashara

Uhispania kwa ushindhi hio imefanikiwa kutetea ubingwa wao ambao iliunyakua miaka minne iliyopita na kuweka rekodi mpya ya kufanikiwa kuifunga Italia kwa mara ya kwanza katika michezoya mashindano.

Dakika kumi na nne zilitosha kwa Uhispania kuweza kuandika goli lake la kwanza kupitia kwa David Silva akiunganisha mpira uliopigwa na Cesc Fabregas na kuifanya kuongoza mapema kabla ya Beki Jordi Alba kufunga goli la pili.

Timu hizo zilienda kupumzika huku Uhispania wakiwa mbele kwa magoli hayo mawili kwa bila dhidi ya Italia lakini kipindi cha pili hali ikazidi kuwa mbaya kwa The Azzuri ambapo waliruhusu magoli mengine mawili.

Magoli mengine mawili ya Uhispania yalikwamishwa nyavuni na Fernando Torres kabla ya Juan Mata hajakamilisha karamu ya timu hiyo na kuwazima kabisa Italia ambao walikuwa wanahisi wangeibuka mabingwa.

Italia ililazimika kucheza ikiwa pungufu kwa wachezaji kumi baada ya kiungo wake Thiago Motta kupata majeruhi baada ya kuumia nyama za misuli yake na kushindwa kuingia mchezaji mwngine baada ya wachezaji wote watatu kuwa wamebadilishwa.

Baada ya mchezo huo Kocha Mkuu wa Uhispania Vicente del Bosque amesema hiki ni kipindi bora kwa soka ya nchi hiyo na ndiyo maana wameweza kupata mafanikio ya kushinda Kombe la Dunia na kutetea Kombe la Mataifa ya Ulaya.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Italia Cesare Prandelli amesema kipigo ambacho wamekipata kutoka kwa Uhispania kitakuwa kimetoa somo kwao na kitawafanya wapate hasira ya kupata mafanikio katika siku za usoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.