Pata taarifa kuu
UHISPANIA-ITALIA-UKRAINE-POLAND

Andres Iniesta achaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 2012

Kiungo wa Timu ya Taifa ya Uhispania ambaye anasukuma gozi kwenye klabu ya Barcelona Andres Iniesta amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka 2012 yaliyotamatika hiyo jana huko nchini Ukraine.

Kiungo wa Timu ya taifa ya Uhispania Andres Iniesta achaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano ya Euro 2012
Kiungo wa Timu ya taifa ya Uhispania Andres Iniesta achaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano ya Euro 2012
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Barani ulaya Eefa Andy Roxburgh ndiya ambaye amemtangaza Iniesta kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo kutokana na mchango wake mkubwa kuisaidia Uhispania kutetea ubingwa wake.

Roxburgh amesema Iniesta amechaguliwa kutokana na kuwa na vigezo kadhaa ikiwemo ni pamoja na ubunifu, soka ya kuvutia pamoja na unyenyekevu ambao ameweza kuuonesha pale anapokuwa uwanjani.

Iniesta ambaye alifunga goli la ushindi kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Uholanzi amekuwa chachu ya ushindi wa Timu yake ya Taifa ya Uhispania kutokana na pasi zake maridhawa ambazo amekuwa akizitoa.

Iniesta pia amechaguliwa kuwa katika Timu ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya ambayo imejumuisha wachezaji ishirini na watatu huku Uhispania ikiwa na wachezaji kumi kwenye kikosi hicho.

Steven Gerrard ndiye mchezaji pekee ambaye amejumuishwa kwenye kikosi hicho akitokea nchini Uingereza na Mkurugenzi wa Uefa Roxburgh amesema amejumuishwa kwa kuwa anavigezo vya kuwa kiongozi na alifanikiwa kuiongoza vyema timu yake.

Zlatan Ibrahimovic na Gerrard wanakuwa wachezaji pekee ambao wamejumuishwa kwenye kikosi hicho ambao timu zao hazikiweza kufuzu kucheza katika hatua ya Nusu fainali ya kombe la Mataifa ya Ulaya mwaka huu.

Uefa imesema wachezaji wengine ambao inathmini mchango wao na namna walivyocheza katika kiwango kizuri kwenye mashindano ya mwaka huu ni pamoja na Cristiano Ronaldo na Andrea Pirlo.

Wachezaji ambao wamejumuishwa kwenye kikosi hicho ni pamoja na Makipa: Gianluigi Buffon (Italia), Iker Casillas (Uhispania), Manuel Neuer (Ujerumani)

Mabeki: Gerard Pique (Uhispania), Fabio Coentrao (Ureno), Philipp Lahm (Ujerumani), Pepe (Ureno), Sergio Ramos (Uhispania), Jordi Alba (Uhispania)

Viungo: Daniele De Rossi (Italia), Steven Gerrard (Uingereza), Xavi (Uhispania), Andres Iniesta (Uhispania), Sami Khedira (Ujerumani), Sergio Busquets (Uhispania), Mesut Ozil (Ujerumani), Andrea Pirlo (Italia), Xabi Alonso (Uhispania)

Washambuliaji: Mario Balotelli (Italia), Cesc Fabregas (Uhispania), Cristiano Ronaldo (Ureno), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), David Silva (Uhispania)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.