Pata taarifa kuu
MAREKANI

Novak Djokovic anyakua taji baada ya kumchachafya Murray

Mchezaji namba moja kwa katika mchezo wa tenisi duniani mchezo Novak Djokovic jana alifanikiwa kunyakua taji la Miami kwa mara ya tatu.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ushindi huo wa Novak Djokovic ulipatikana baada ya kumshinda raia wa Uingereza Andy Murray katika mchezo waliotumia saa 2 na dakika 18 mchezo ambao ulipigwa mjini Miami nchini Marekani.

Novak Djokovic raia wa Serbia alishinda mchezo huo kwa seti za 6-1, 7-6 na 7-4 na hivyo kunyakua taji hilo ambalo yeye anaona ni kitu cha kujivunia lakini pia ni dalili ya kuonyesha ubora wake.

Mwaka 2009 katika fainali ya michezo hiyo Andy Murray alimshinda Novak Djokovic lakini mwaka huu mambo yakawa kinyume.

Novak Djokovic amesema kuwa mchezo huo ulikua mgumu na hali ya hewa haikuwa nzuri lakini jitihada zake ndizo zilizompa ushindi huo.

Kwa upande wake Murray alisifu mchezo wa mpinzani wake na kusema kuwa alicheza mchezo mzuri zaidi yake na alistahili kushinda.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.