Pata taarifa kuu
MEXICO

Morales aachia taji kwa kushindwa kukidhi viwango vya uzito.

Mwanamasumbwi wa Mexico Erik Morales amepoteza taji lake la baraza la masubwi duniani katika uzito wa kati, baada ya kuongeezeka uzito zaidi ya kiwango kinachotakiwa cha paundi 140 katika pambano lake la leo Jumamosi dhidi ya Danny Gracia.

bestboxingblog.com
Matangazo ya kibiashara

Morales amebainika kuwa na uzito wa paundi 142 baada ya kupimwa uzito katika mzani , jambo ambalo limedhihirisha kuwa hawezi kutetea tena taji lake hilo hata kama atamshinda mpinzani wake na mwanamasumbwi asiyeshindwa kutoka Marekani Danny Gracia.

Gracia ambaye anauzito wa paundi 139.5 bado analazimika kumpiga Morales ili aweze kutwaa taji hilo tofauti na hivyo taji hilo litabaki kuwa wazi.

Mchezo kati ya Morales na Gracia umekuwa ukicheleweshwa tangu mwezi Januari ili kumwezesha Morales kufanyiwa upasuaji wa kibofu cha nyongo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.