Pata taarifa kuu
UINGEREZA-UHOLANZI

Stuart Pearce akiri kutoweza kuwa Kocha wa Uingereza kwa muda mrefu

Kocha wa Muda wa Timu ya Taifa ya Uingereza Stuart Pearce amesema atakuwa na furaha zaidi kama ataiongoza timu hiyo kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya zitakazofanyika baadaye mwaka huu lakini hana nia ya kuchukua kazi hiyo kwa muda mrefu.

Kocha wa Muda anayekinoa Kikosi Cha Timu ya Taifa ya Uholanzi Stuart Pearce
Kocha wa Muda anayekinoa Kikosi Cha Timu ya Taifa ya Uholanzi Stuart Pearce
Matangazo ya kibiashara

Pearce amesema kuwa ana imani jukumu la kuiongoza Uingereza maarufu kama Three Lions ataliweza kwenye Mashindano ya Euro 2012 lakini hategemei kuchukua jukumu hilo kwa muda mrefu kama wengi wanavyodhani.

Kocha huyo wa muda amesema hana uhakika kama anauzoefu wa kutosha kuweza kukinoa kikosi cha Uingereza kwa muda mrefu kwa kuwa Timu hiyo inahitaji Kocha mwenye uzoefu wa kutosha hasa kwenye mashindano makubwa.

Pearce ambaye alikuwa Msaidizi wa kocha Mkuu aliyejiuzulu wadhifa wake Fabio Capello amesema kwa sasa yupo lakini anajua fika Chama Cha Soka nchini Uingereza FA kipo katika mchakato wa kusaka kocha mpya.

Kauli ya pearce ameitoa baada ya kufanikiwa kuiongoza Uingereza kwenye mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Uholanzi ambayo aliambulia kichapo cha magoli 3-2 kwenye mchezo ulipigwa kwenye Dimba la Wembley.

Pearce amejikuta akipoteza mchezo huo kwa goli lililopachikwa kimiani na Arjen Robben baada ya hapo awali kutoka nyuma kwa magoli mawili na kufanya mchezo kuwa sare kupitia magoli ya Gary Cahill na Ashley Young.

Kwenye mchezo huo Uingereza imepoteza wachezaji watatu kutokana na kupata majeruhi akiwemo Beki wa kati ya Manchester United Chris Smalling, Nahodha wa Liverpool Syeven Gerrard na Winga wa Chelsea Daniel Sturridge.

Uholanzi kwenye mchezo huo ilipata magoli yake kupitia kwa Arjen Robben ambaye alifunga mara mbili kwenye dimba hilo la Wembley huku Klaas Jan Huntelaar ambaye alishindwa kumaliza mchezo huo akifunga goli moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.