Pata taarifa kuu
TANZANIA

Yanga yakubali sare ya bao 1-1 dhidi ya Zamalek.

Timu ya Young Africans ( Yanga) ya Tanzania ikiwa nyumbani imekubali sare ya goli 1-1 dhidi ya timu ya Zamalek kutoka misri katika mtanange wa ligi ya mabingwa Afrika uliochezwa hapo jana katika dimba la taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Yanga
Matangazo ya kibiashara

Katika mtanange huo timu ya Yanga ilionekana kutawala mchezo huku ikikosa magoli kadhaa ya wazi kabla ya kupata bao moja ambalo hata hivyo lilisawazishwa na Zamalek baada ya kutokea uzembe kwa upande wa mabeki wa timu ya Yanga.

Wakati Yanga wakiwa wenyeji wa Zamalek, watani wao Simba walikuwa ugenini kumenyana na timu ya Kiyovu ya nchini Rwanda katika kombe la shirikisho ambapo hadi kipenga cha mwisho timu hizo zimetoshana nguvu baada ya kutoka sare ya goli 1-1.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.