Pata taarifa kuu
Marekani

Serena Williams ajiondoa mashindano ya tenesi ya Monterrey.

Nyota wa tenesi nchini Marekani Serena Williams amejiondoa katika mashindano ya Monterrey yanayotaraji kufanyika juma lijalo kutokana na jeraha alilopata kwenye kiwiko cha mguu waandaaji wa mashindano hayo wamearifu.

Bingwa wa zamani wa tennesi duniani Serena Williams
Bingwa wa zamani wa tennesi duniani Serena Williams AFP
Matangazo ya kibiashara

Bingwa huyo wa zamani wa dunia amepata mwaliko wa mashindano hayo yanayoanza kesho Jumatatu.

Hata hivyo waandaaji wa mashindano hayo wamesema kuwa wamepokea taarifa kutoka katika chama cha mchezo wa tenesi duniani WTA zikisema kuwa Serena hatoweza kukubali mwaliko huo kutokana na hali yake ya jeraha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.