Pata taarifa kuu

Timu za Tanzania Yanga na Simba zashuka dimbani michuano ya kimataifa

Timu za Simba na Yanga za Tanzania mwishoni mwa juma hili zitakuwa zikishuka dimbani kwenye michezo ya kimataifa zikisaka nafasi za kusonga mbele katika michuano hiyo ya kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Katika harakati hizo mabingwa wa Tanzania Yanga watakuwa wenyeji wa Zamalek toka Misri kwenye uwanja wa taifa katika ligi ya mabingwa Afrika.

Watani zao simba watakuwa wakicheza kombe la shirikisho huko nchini Rwanda kuivaa Timu ya Kiyovu.

Mashabiki wa Simba wameonekana kununua jezi za Zamalek kwa nia ya kuishangilia timu hiyo viongozi wa Simba na Yanga walijaribu kuzungumza na mashabiki wao ili timu zao zinapocheza mechi za kimataifa wawe kitu kimoja lakini juhudi hizo zilikuwa kama kupaka upepo rangi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.