Pata taarifa kuu
Uingereza

Stuart Pearce ateuliwa na FA kuiongoza Uingereza katika mechi ya kirafiki na Uholanzi

Stuart Pearce atashika nafasi ya Fabio Capello, katika Mechi ya Kirafiki kati ya Uingereza na Uholanzi tarehe 29 Mwezi huu. 

Stuart Peace ambae ameteuliwa kuiongoza timu ya soka ya Uingereza katika mechi ya kirafiki na Uholanzi
Stuart Peace ambae ameteuliwa kuiongoza timu ya soka ya Uingereza katika mechi ya kirafiki na Uholanzi
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu, David Bernstein hii leo amemteua Pearce ambaye ni Kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza ya vijana wa Umri wa chini ya miaka 21.

Shirikisho la soka nchini Uingereza, limeanza Mchakato wa kuanza kumpata Kocha mpya wa timu ya Taifa ya Uingereza baada ya Fabio Capello kujiuzulu wadhifa huo kufuatia sakata la John Terry.

Kumekuwa na tetesi kuwa huenda Kocha wa tottenham hotspur, Harry Redknapp akamrithi Capello aliyejiuzulu usiku wa jana baada ya kuukosoa hadharani uamuzi FA kumvua unahodha Mchezaji wa Chelsea, John Terry.

Uamuzi wa Capello wa kushtukiza umefanyika wakati ambapo pia Kocha wa Tottenham kukutwa hana hatia na mahakama ya Southwark alipokuwa akikabiliwa na shutma za kukwepa kulipa Kodi.

FA itafanya mkutano na waandishi wa Habari hii leo ili kumteua mrithi kabla ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, michuano itakayopigwa Miezi minne ijayo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.