Pata taarifa kuu
Gabon

Safari ya kufuzu Gabon na Equatorial Guinea mwishoni mwa Juma hili

Mataifa mbalimbali barani Afrika yanashiriki katika mechi kadhaa za soka wikendi hii, katika kinyanganyiro cha kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika mwaka ujao, huko Equatorial Guinea na Gabon.Katika kundi J, Harambee Stars ya Kenya, inakabiliwa na kibarua kigumu huko mjini Luanda Jumapili, hii watakakovaana na Angola.

Uwanja wa mpira wa miguu wa Wydad Casablanca
Uwanja wa mpira wa miguu wa Wydad Casablanca TheJaberian
Matangazo ya kibiashara

Safari ya Harambee Stars imekumbwa na matatizo ya hapa na pale kutokana na kikosi cha Kenya kukosa uwanja wa kufanyia mazoezi, licha ya kuwasili Angola mapema mno kwa maandalizi ya mchuano wao.

Jijini Kampala, Jumamosi hii Uganda Cranes wanaogoza kundi hilo kwa pointi saba na wanawakaribisha Guinea Bissau ambayo ni ya tatu kwa alama tatu.

Taifa Stars ya Tanzania iko ugenini jijini Bangui, wanakopambana na wenyeji wao Jamhuri wa kati, katika mchuano wa Jumamosi ambao vijana wa Jean Poulsen kutoka Denmark wanacheza bila ya wachezaji wao wa kutegemewa Henry Joseph ambaye anauguza majeraha na Dan Mrwanda na Abdi Kassim, ambao klabu yao iliwanyima nafasi ya kujiunga na kambi ya stars.

Tanzania ni ya pili katika kundi lao kwa pointi nne ikimfuata mwenyeji wake Afrika ya Kati anayeongoza kundi hilo, wakati Morroco na Algeria ambazo zote pia zina pointi nne zinafuata;.

Chipolopolo ya Zambia nayo inacheza na Msumbiji jijini Lusaka,huku wapenzi wa soka nchini Burundi wakisubiri mchuano kati ya mahasimu wao wa jadi ,Amavubi Stars ya Rwanda jijini Bunjumbura.

Katika kundi hilo, Benin ambayo inacheza na Cote Dvoire,inaongoza kwa alama nne,mbele ya Rwanda ni ya pili kwa alama tatu, huku Burundi ikifunga mkia kwa alama moja.

Ghana wanamenyana na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, huku Bostwana wakiwaanda Malawi.

Michuano mingine inayosakatwa wikendi hii ni pamoja na Ethiopia dhidi ya Super Eagles ya Nigeria, Cameroon na Senegal huku Misri wakiwandaa Afrika Kusini huko Cairo.

Bostwana, tayari wamefuzu katika fainali hiyo kwani hadi sasa wana alama 16 katika kundi K, kwa kushinda mechi zao zote.

Washindi wa kwanza na wa pili watafuzu kushiriki katika kindumbwendumbwe hicho, nchini Gabon na Equitorial Guinea mwakani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.