Pata taarifa kuu
Uswizi

Sepp Blatter asema hana kinyongo na FA kwa kutompigia kura.

Baada ya kuchaguliwa tena kuongoza kandanda ulimwenguni jana, rais wa FIFA Sepp Blatter amesema kuwa hana kinyongo na Shirikisho la Soka la Uingereza FA, lililotaka uchaguzi huo uahirishwe.

Rais mteule wa Fifa, Sepp Blatter
Rais mteule wa Fifa, Sepp Blatter
Matangazo ya kibiashara

Blatter amesema kuwa kura 168 alizozipata katika uchaguzi wa jana ,zinadhihirisha wazi kuwa yeye ndiye rais wa mashirikisho yote duniani na hatalitenga shirikisho lolote katika utendakazi wake.
Baada ya ushindi huo, Blatter alijiita jana kama NAHODHA wa kandanda ulimwenguni.
Waziri Mkuu wa Urusi Vladimir Putin, ambaye taifa lake litakuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2018, amemsifu Blatter kwa kuchaguliwa tena na kumwombea mema katika uongozi wake wa miaka minne ijayo.
 

Blatter mwenye umri wa miaka 75 na ambaye amekuwa rais wa FIFA tangu mwaka wa 1998, ameahidi kuongoza mabadiliko muhimu katika shirikisho hilo, ikiwa ni pamoja na viongozi wa vyama vya soka kote duniani, kushiriki katika zoezi la kuchagua mwenyeji wa kombe la dunia na halikadhalika kuifanya kamati ya maandalizi kuwa huru zaidi na kufanya kazi yake bila ya kuingiliwa na yeyote yule.
 

Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka wa 2022, na Urusi mwaka 2018 kulisababisha mgogoro katika shirikisho hilo, huku tuhuma zikiibuka kuwa rushwa ilitumiwa kupata mataifa hayo, hasa Uingereza na Mareakani zikiishutumu FIFA kwa kuyapa mataifa hayo mawili kuwa wenyeji wa mashindano hayo ya kombe la dunia.
 

Blatter sasa, atakuwa uongozini kwa miaka minne ijayo, na ameahidi kuwa atatoa uongozi bila kupendelea mashirikisho yote ya soka kote duniani, licha ya Shirikisho la soka la Uingereza kususia kushiriki katika uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.