Pata taarifa kuu
Switzerland

Sepp Blatter asema FIFA haipo katika malumbano

Rais wa FIFA Sepp Blatter,amesema kuwa shirikisho hilo la soka haliko katika mgogoro wowote bali ni matatizo ya hapa na pale ambayo anasema yatateuliwa na wajumbe wa FIFA.

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, anayeondoka madarakani Joseph Blatter.
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, anayeondoka madarakani Joseph Blatter. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Blatter amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana jioni katika makao makuu ya FIFA huko Zurich Uswizi, kujibu tuhuma za ufisadi zinazolikumba shirikisho hilo, katika siku za hivi karibuni.
Mkutano mkuu wa FIFA,unaanza baadaye leo huko Zurich kabla ya uchaguzi wa urais kufanyika kesho Jumatano ambapo Blatter anatarajiwa kuchaguliwa au kupitishwa moja kwa moja na wajumbe 208 kwani hana mpinzani katika kinyanyiro hicho.
Mpinzani wake Blatter Mohhamed Bin Hamam kiongozi wa shirikisho la soka barani Asia alijiondoa katika uchaguzi huo baada ya tuhma kuwa alitoa fedha kama hongo za kutaka kura kutoka kwa wajumbe wa visiwa vya Carrebian .
Sepp Blatter ambaye amekuwa katika shirikisho hilo kwa muda wa mia 36 sasa, na kuongoza FIFA kama rais tangu mwaka wa 1998, alionekana mwenye hasira na kusema kuwa hatima yake inasalia mikononi mwa wajumbe wa FIFA, wala sio serikali au mtu yeyote nje na FIFA.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.